Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akikata keki na kuzindua kikundi
cha Wanawake Chuma katika Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano -Picha - Malunde
Mamía
ya wanawake wamejitokeza kushiriki Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa
Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi wa Malex uliopo Kahama,
mkoani Shinyanga, huku wito ukitolewa kwa wanawake kushirikiana na
kuinua wenzao ili kufikia mafanikio ya pamoja.
Mgeni
rasmi katika tamasha hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni
Mhita, aliyesisitiza umuhimu wa mshikamano, uthubutu na kujiamini kwa
wanawake katika harakati za maendeleo binafsi na ya jamii.
Akizungumza
katika tamasha hilo, Mhita amewataka wanawake kuacha hofu ya maneno ya
watu na badala yake kuzingatia malengo yao kwa vitendo.
“Mwanamke
hakikisha unapambana ili kufikia malengo yako, usiogope kusemwa. Wewe
songa mbele kwa sababu uwe mzuri utasemwa, uwe mbaya utasemwa, upendeze
utasemwa, usipendeze utasemwa. Kuna watu wamevunjika moyo kwa sababu ya
kusemwa, hakikisha kuwa upo na watu sahihi, jiamini, usihangaike na watu
wenye kukutisha tamaa. Ili mwanamke uonekane umefanikiwa, lazima uinue
wanawake wenzako. Uwe nguzo ya kuwainua wengine,” amesema Mhita.
Akifafanua
zaidi, Mhita amebainisha kuwa katika dunia ya sasa, mafanikio ya
mwanamke yanategemea zaidi uthubutu wa kiuchumi, akisisitiza kuwa, “siri
ya mwanamke yoyote ni sasampa (pesa), na habari ya mjini ni pesa, hivyo
ni lazima mwanamke uhakikishe unazitafuta na kuzitumia fursa
zinazokuwezesha kuinuka kiuchumi.”
Ameongeza
kuwa wanawake wanapaswa kujiamini na kutumia kikamilifu fursa
zilizowekwa na serikali, ikiwemo mikopo na uwezeshaji katika sekta
mbalimbali kama madini, kilimo na viwanda, akibainisha kuwa mazingira
rafiki yameboreshwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema
kuwa kupitia maboresho hayo, wanawake wachimbaji wa madini sasa
wanapata mikopo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji,
huku sekta ya kilimo ikipewa kipaumbele kwa kuongeza bajeti ili wanawake
wanufaike zaidi.
Aidha,
ameeleza kuwa hata katika sekta ya viwanda wanawake wameendelea
kunufaika na fursa zilizopo na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Mhita
amewapongeza wanawake wa Ushetu kwa jitihada zao katika kusindika na
kuongeza thamani ya mazao, akieleza kuwa huo ni mfano bora wa namna
wanawake wanavyoweza kutumia fursa za kiuchumi kujiletea maendeleo
endelevu.
Pia
amegusia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya afya na elimu,
akieleza kuwa Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi,
huku Mkoa wa Shinyanga ukiwa sasa na shule sita za wasichana, hatua
inayochochea upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike na kumjengea msingi
imara wa mafanikio ya baadaye.
Akisoma
risala kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Gold FM na mwandaaji wa tamasha
hilo, Bi. Neema Mghen, amesema Tamasha la Mwanamke Chuma limeendelea
kuwa zaidi ya tukio la kawaida na sasa ni jukwaa muhimu la mabadiliko
kwa wanawake.
Neema Mghen
Amesema
kupitia tamasha hilo, wanawake wengi wamefanikiwa kujikwamua kiuchumi,
kujitambua, kujiamini na kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi
na maamuzi ndani ya familia na jamii.
Kaulimbiu ya mwaka huu, “Nguvu ya Ujasiri,”
imelenga kuhamasisha wanawake kusimama bila uoga, kuchukua hatua na
kutumia fursa zilizopo kubadilisha maisha yao na ya wengine.
Ametaja
mafanikio ya msimu wa tano kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kikundi cha
Mwanamke Chuma Maendeleo Group kilichozinduliwa rasmi wakati wa Tamasha
la Mwanamke Chuma 2026, kusaidia wanawake wa gereza la Kahama kwa
kuwapatia mahitaji muhimu, pamoja na kuendeleza utamaduni wa kutoa tuzo
kwa wanawake ili kutambua na kuhamasisha juhudi zao.
Hata
hivyo, amebainisha changamoto zinazowakabili wanawake kuwa ni pamoja na
ukosefu wa mitaji na utaalamu katika sekta ya uchimbaji mdogo wa
madini, uwepo wa mikopo yenye riba kubwa na masharti magumu, pamoja na
changamoto za pembejeo bora na masoko ya uhakika katika sekta ya kilimo.
“Tunaamini
ukimuinua mwanamke, umeinua familia na jamii kwa ujumla. Ujasiri wa
mwanamke si kelele bali ni hatua, si maneno bali ni matendo,” amesema Mghen.
Ameongeza
kuwa Tamasha la Mwanamke Chuma lina lengo la kukuza uchumi wa wanawake
mmoja mmoja na vikundi, kujenga mshikamano, uthubutu na kuimarisha sauti
ya pamoja ya wanawake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Katika
tamasha hilo lililoandaliwa na Kituo cha Redio cha Gold FM, viongozi
mbalimbali wamehudhuria akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP
Janeth Magomi, Mbunge wa Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani na Mbunge wa
Kahama Mjini Mhe. Benjamini Ngayiwa, pamoja na wadau mbalimbali wa
maendeleo.

Tamasha
hilo limepambwa na burudani kutoka kwa msanii mkongwe wa muziki wa
taarab, Mzee Yusuph, huku uendeshaji wa shughuli ukifanywa na MC maarufu
Dkt. Kumbuka na mtaalamu wa maendeleo ya familia na uchumi, Dkt. Chris
Mauki, aliyetoa mada mbalimbali zilizolenga kuwainua wanawake kiuchumi
na kijamii.
Aidha,
jumla ya tuzo tisa za ushindani zimetolewa kwa washindi waliopatikana
kupitia kura za wananchi, pamoja na tuzo maalum za heshima na vyeti kwa
wadau waliotoa mchango mkubwa katika kuwawezesha wanawake.
Tuzo
hizo zimetolewa kwa wanawake waliobobea katika nyanja mbalimbali
zikiwemo ujasiriamali, madini, ubunifu, ushonaji, upishi, saluni pamoja
na wanawake wenye ushawishi chanya katika jamii, hatua inayolenga
kuhamasisha wanawake wengine kujituma na kufikia mafanikio.
ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Tamasha la
Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi
wa Malex uliopo Kahama, mkoani Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Tamasha la
Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026 katika Ukumbi
wa Malex uliopo Kahama, mkoani Shinyanga - Picha na Kadama Malunde

Mwanamke Chuma Msimu wa Tano lililofanyika Aprili 11, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akiimba na kucheza na Wanawake Chuma kwenye Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akiimba na kucheza na Wanawake Chuma kwenye Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizindua kikundi cha Wanawake Chuma katika Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano

wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akikabidhi katiba ya kikundi cha
Wanawake Chuma katika Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akikata keki katika Tamasha la Mwanamke Chuma Msimu wa Tano

Mwandaaji
wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha
Redio cha Gold FM, Bi. Neema Mghen akisoma risala kuhusu Tamasha la
Mwanamke Chuma
Mwandaaji
wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha
Redio cha Gold FM, Bi. Neema Mghen akisoma risala kuhusu Tamasha la
Mwanamke Chuma
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza katika Tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza katika Tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Benjamini Ngayiwa akizungumza katika Tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Mwandaaji
wa Tamasha la Mwanamke Chuma 2026 ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha
Redio cha Gold FM, Bi. Neema Mghen akikabidhi tuzo ya Heshima kwa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Shinyanga SACP Janeth Magomi
Mtaalamu wa maendeleo ya familia na uchumi, Dkt. Chris Mauki akitoa mada kwenye tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Mtaalamu wa maendeleo ya familia na uchumi, Dkt. Chris Mauki akitoa mada kwenye tamasha la Mwanamke Chuma 2026
Msanii Mkongwe wa Taarabu, Mzee Yusuph akitoa Burudani

Msanii Mkongwe wa Taarabu, Mzee Yusuph akitoa Burudani

Chapisha Maoni