Mbunge
wa Jimbo la Msalala Mhe Mabula J. Magangila
Mbunge
wa Jimbo la Msalala Mhe Mabula J. Magangila Aprili 12.4.2026 alihitimisha ziara yake ya siku mbili katika Kata ya Bulyanhulu kwa kufanya
mkutano wa hadhara.
Aidha,
alisikiliza kero za wananchi na kusisitiza dhana ya uwajibikaji wa
pamoja kwa viongozi wote ili kuweza kutatua changamoto za wananchi
ikiwa ni pamoja na kusoma mapato na matumizi kwa wananchi.
Ziara hiyo ilihudhuriwa na Watumishi wa taasisi za serikali na viongozi
wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Cde Odilia Batimayo na Diwani wa Kata ya Bulyanhulu Mhe Musingi
Sabaganga.
Imetolewa na: Ofisi ya Mbunge, Msalala. |
Chapisha Maoni