MAGANGILA ASHIRIKI UZINDUZI WA MSALALA VETERANS JOGGING CLUB

 

Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe Mabula Johnson Magangila akiwa na wanamichezo wa kikundi cha Msalala Veterans Jogging club alipokuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Club hiyo. 



Aidha, alisisitiza wana-Msalala wote kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kuimarisha afya lakini pia ameeleza kuwa adhima yake ni kuhakikisha sekta ya michezo inageuka chanzo cha uchumi kwa vijana.

Sambamba na hilo Mhe Mbunge aligawa vifaa vya michezo kama jezi na mpira kwa Timu sita zilizofika kushiriki pia uzinduzi huo.


Uzinduzi huo, ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Mwenyekiti wa ÚVCCM Mkoa wa Shinyanga Cde Benson Werema.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge, Msalala 
12.4.2026

0/Post a Comment/Comments