Mkuu
wa wilaya ya Ukerewe, Mhe. Christopher Ngubiagai
(aliyesimama),akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waganga wa tiba
asili na tibambadala yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu
waSerikali. Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili kuanzia Machi 26
hadi 27, 2026. Kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, John Wanjala
na kushotoni Kaimu Meneja wa Maabara ya Chakula na Dawa, Everlight
Matinga.
**********
Serikali
kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeendelea
kuonesha dhamira ya kuinua sekta ya tiba asili nchini baada ya kuzindua
mafunzo ya uchakataji salama wa dawa asili kwa waganga wa tiba asili na
tiba mbadala kutoka mikoa ya Mara, Simiyu na Mwanza.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Machi 26, 2026
Ukerewe, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, alisema
serikali inatambua mchango mkubwa wa waganga wa tiba asili katika utoaji
wa huduma za afya kwa Watanzania, huku akisisitiza kuwa mafunzo hayo ni
sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Afya inayotambua rasmi tiba
asili na tiba mbadala hapa nchini.
“Serikali
imewaleta wataalamu wa GCLA ili kuhakikisha dawa za asili zinachakatwa
kwa viwango vinavyokubalika, zinakuwa salama na zenye ubora unaoweza
kushindana hata katika masoko ya kimataifa,” alisema Ngubiagai.
Aidha,
Ngubiagai Aliongeza kuwa jitihada hizo pia zinalenga kurasimisha sekta
ya tiba asili na kuwajengea uwezo waganga hao ili waweze kuwa sehemu ya
mfumo rasmi wa huduma za afya nchini, hatua itakayoongeza heshima na
uwajibikaji wao katika jamii, ambapo pia alihusisha mafunzo hayo na Dira
ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, akibainisha kuwa tiba asili ina
mchango mkubwa katika kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora, kukuza
uchumi shindani unaotumia rasilimali za ndani pamoja na kuchochea
ubunifu na ajira.
Katika
hatua nyingine, Ngubiagai alisisitiza umuhimu wa kuzingatia misingi ya
uchakataji salama ikiwemo usafi wa mazingira ya utayarishaji, matumizi
ya vipimo sahihi vya dawa, ufungashaji bora pamoja na ushirikiano na
wataalamu wa afya ili kuepuka madhara kwa watumiaji huku akiweka wazi
kuwa tiba asili inaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato kupitia biashara
na hata utalii wa tiba endapo ubora wake utaimarishwa na kuwekewa
viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
Akimwakilisha
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, Meneja wa Kanda ya
Ziwa, John Wanjala, alisema kuwa lengo la Mamlaka ni kuhakikisha dawa
zote zinazozalishwa zinakuwa salama, bora na zenye uwezo wa kushindana
katika soko la ndani na nje ya nchi huku akieleza kuwa mafunzo hayo
yanalenga kuwasaidia waganga wa tiba asili kuendana na mabadiliko ya
sayansi na teknolojia, ikiwa ni pamoja na kuboresha uzalishaji na
kupanua masoko ya bidhaa zao.
“Popote
walipo waganga wa tiba asili, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali tutaendelea kuwafikia kwa mafunzo na huduma za kitaalamu ili
kuhakikisha wanatoa huduma zilizo bora na salama kwa jamii,” alisema
Wanjala.
Kwa
upande wake Katibu wa chama cha Tiba Asili na Tiba Mbadala (TAMESOT),
Maneke Malegeli, akizungumza kwa niaba ya washiriki, aliishukuru Mamlaka
kwa mafunzo hayo kwa kuwa yamewasaidia kupata uelewa wa mbinu bora za
utengenezaji, utayarishaji na ufungashaji wa dawa asili kwa kuzingatia
viwango vinavyolinda afya za watumiaji na kuongeza kuwa mafunzo hayo pia
yatawasaidia kujitofautisha na matapeli wanaotumia jina la tiba asili
vibaya, huku pia akiiomba Mamlaka kuendelea kutoa elimu hiyo ili iweze
kuwafikia waganga wengi zaidi nchini.
Waganga
wa tiba asili na tiba mbadala kutoka Ukerewe, wakimsikilizamgeni rasmi
(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo hayo ya siku mbili.
Meneja
wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Kanda ya
Ziwa, John Wanjala, akiwasilisha mada kuhusu mbinu bora za uzalishaji na
usafi wa dawa za tiba asili kwenye mafunzo yaliyofanyika Ukerewe,
mkoani Mwanza.
Mkuu
wa wilaya ya Ukerewe, Mhe. Christopher Ngubiagai (katikati), akipokea
zawadi kutoka kwa Mlezi wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili - Ukerewe,
Makubi Makubi baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mtumishi
wa Mamlaka, Lulu Kiwia, akifafanua jambo kuhusu aina yauchunguzi wa
kimaabara unaofanyika kwenye dawa asili wakati wamafunzo kwa waganga wa
tiba asili na tiba mbadala yaliyofanyika wilayaniUkerewe.
Kaimu Meneja wa Maabara ya Chakula na Dawa, Everlight Matingaakiwasilisha mada kuhusu vifungashio vya dawa asili.
Mshiriki
wa mafunzo, Consolata Nabina, akichangia hoja kuhusuufangushaji na
uhifadhi wa dawa wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyikaUkerewe.
Katibu
wa Chama cha Tiba Asili na Tiba Mbadala (TAMESOT), ManekeMalegeli,
akiandika maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya (hayupopichani) wakati
akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika Ukerewe, Mwanza.
Mkuu
wa wilaya ya Ukerewe, Mhe. Christopher Ngubiagai (katikati), akiwana
viongozi kutoka Mamlaka pamoja na washiriki wa mafunzo ya
uchakatajisalama wa dawa asili, waganga wa tiba asili na tiba mbadala
mara baada yakufungua mafunzo kwa wataalam hao wa tiba asili na tiba
mbadala.









Chapisha Maoni