Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J.
Maulid, amefanya kikao kazi na watumishi wa taasisi hiyo kutoka kampasi
zote, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, umoja na mshikamano katika
kufanikisha malengo ya taasisi.
Akifungua
kikao hicho, Dkt. Maulid mesema kuwa watumishi wanapaswa kuwajibika
kikamilifu katika nafasi zao huku wakidumisha mshikamano ili kuongeza
ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
“Tunapaswa
kuwajibika kwa nafasi zetu kwa kuwa wamoja na wenye mshikamano ili
kuleta tija katika utimizaji wa malengo ya taasisi,” amesema Dkt.
Maulid.
Katika
kikao hicho, watumishi wapya waliojiunga na ADEM kutoka taasisi
mbalimbali walipata fursa ya kujitambulisha, ambapo waliaswa kufanya
kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma ili kuchangia maendeleo ya taasisi
hiyo.
Kwa
upande wake, Dkt. Lucas Mzelelela amesisitiza umuhimu wa watumishi
kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa bidii na
nidhamu wakati wote wawapo kazini.
“Kila
mtumishi anapaswa kutumikia kiapo chake cha utumishi wa umma kwa
kuwajibika ipasavyo na kuwa na nidhamu ya kazi kwa muda wote wawapo
kazini,” amesema Dkt. Mzelelela.















Chapisha Maoni