UMUHIMU WA KUVAA SAA ZA MKONONI.


leo tutajaribu kuongalia sababu kwanini tunatakiwa tuvae saa za mkoni yaani nini haswa kinatulazimisha kuvaa saa za mkononi , hebu kwanza tujue saa za mkononi zilianza kuvaliwa mwaka gani.

Kabla ya vita ya kwanza ya dunia kulikuwa kuna saa za mfuko yaani pocket watch saa hizi zilipendwa sana enzi hizo. ila katika kipindi cha mapigano wanajeshi walihitaji saa ambayo itakuwa rahisi kuangalia sio mpaka watoe mfukoni hivyo walianza kuvaaa saa mkononi na ikawa rahisi sana kuangalia wakati wa mapigano ..na vita ilivyoisha saa ikaonekana ni style sasa ikabidi watu waanze kuvaa kama fashion mitaani huko ulaya. 
sasa tuje sababu zinapelekea wewe au mimi kuvaaa saa japo simu zipo.

SAA HUTUNZA MUDA VIZURI;

Japo kuna simu kuna computer hakuna kifaa kinachopita saa kwa utunzaji mzuri wa muda hasa saa za mabattery ya quartz za mwaka 1955 pia saa ya mkononi humpa mtu urahisi wa kuangalia wakati muda wowote atakao pia kuanza kufungua mfuko au bag.

SAA ZINA NGUVU MBALIMBALI;

Saa mara nyingi huwa zina sifa mbalimbali kama uwezo wa kutoingia maji hivyo kufanya mtumiaji kuvaa popote atakapo hata kwenye maji kuna zingine ni ngumu kupasuka yaani shock resistant hasa kwa saa za kampuni ya gshocK au skmei

SAA HAZIITAJI KUCHARGE’;

Kama tulipo sema saa ni simple sana hautaji wewe kuichaji maana kuna saa ambazo battery hukaa hata miaka mitano bila kuisha hasa saa za kijapani, pia kuna saa ambazo huwa hazitumii kabisa battery hizi huenda na mawimbi ya mkono wako. Japo Kwa sasa zipo baadhi ya saa zinazochajiwa.



SAA NI FASHION;

Saa za mkononi pia ni fashion huongeza umaridadi na urembo wa mtumiaji au mmiliki wa saa husika. katika vitu wataalam wa fashion huwa wanashauri ni kuvaa saa mkononi ukitaka upendeze zaidi na mavazi yako wewe vaa saa ya mkononi muonekano wako utaongeza na utang’ara zaidi pia ili tupendeze kitaa au maofisini wakuu saa ni muhimu.

SAA HUTENGENEZA UHUSIANO KATI YA WEWE;

Asikwambie mtu watu wanao vaa saa mara nyingi huwa ni matime keeper wazur pia hujali muda wao tena ngoja nikukumbushe ndugu yangu we umeshahau kipindi tunasoma matime keeper wote walichagulia kisa anamiliki saa tu tena saa nzuri.. hivyo mara nyingi ukimiliki saa automatic utautunza muda wako sahihi ndugu yangu.

0/Post a Comment/Comments