Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel.
Na Dotto Mwaibale, Arusha
Umoja
wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) unatarajia kuwakutanisha wanamuziki,
wananchi, viongozi na wadau mbalimbali katika Tamasha kubwa
litakalohusu mchango wa wanamuziki katika maendeleo ya nchi ambalo
litafanyika kwa siku tatu jijini Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel amesema
maandalizi yote yamekamilika na kuwa kwaya mbalimbali na wanamuziki
binafsi watakuwepo kutoa burudani.
"Tamasha
hilo litakuwa la siku tatu na litafanyika katika Makumbusho ya Taifa ya
Elimu Viumbe Arusha jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa kuanzia Agosti 25
hadi Agosti 27, 2023" amesema Joel.
Amesema
makundi ya kwaya na waimbaji binafsi watakuwepo kutoa burudani
wakiongozwa na kwaya Kuu Habari Njema ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) na Kwaya ya Tangazeni ya kanisa hilo Unga Limited zote
za jijini Arusha.
Amesema
pia kutakuwa na bendi kutoka mikoa mbalimbali ambazo zitashiriki kutoa
burudani kwenye tamasha hilo kubwa na la aina yake.
Ametaja
kundi lingine ambalo litakuwepo ni wadau wa maendeleo ambapo pia
kutakuwepo na fursa mbalimbali na kuwa kiingilio ni bure.
Joel
ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wa
muziki kufika kwenye tamasha hilo ambapo aliwataja baadhi ya wadau
watakao kuwepo kuwa ni pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Hifadhi |Dodoma ], Dkt.Noelia Myonga, Agness Kanuty, Mwenyekiti wa
Nokongo, Dkt. Lilian Badi na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Elimu
Viumbe Arusha, Dkt. Christina Ngereza.
Mlezi
wa TAMUFO Dkt. Frank Richard amesema katika tamasha hilo Baraza la
Sanaa Tanzania (BASATA) na COSOTA na TAMRISO watakuwepo kutoa elimu na
usajili wa wanamuziki.
Mlezi wa TAMUFO, Dkt. Frank Richard.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi Dodoma, Dkt.Noelia Myonga.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha, Dkt. Christina Ngereza.




Chapisha Maoni